Nahodha wa Yanga SC, Lamine Moro ameongelea ishu ya utovu inayomkabili katika klabu yake baada ya kuwa na maneno mengi yanayoendelea kumuhusu na kuondoshwa katika kikosi katika mchezo dhidi ya Namungo.

“Wiki iliyopita kabla hatujasafiri kwenda Mtwara nilipata majeraja ambayo benchi la ufundi walikuwa wakifahamu, kwa hiyo tulipofika Mtwara, sikuweza kufanya mazoezi lakini nilikuwepo kwenye uwanja wa mazoezi pamoja na timu nzima.” alisema Lamine.

Kocha aliuliza madaktari kwa nini sifanyi mazoezi, akaambiwa kuhusu hali yangu kwamba nimepata majeraha. Kocha alisisitiza kwamba nilitakiwa kufanya mazoezi, nikamweleza kuhusu hali yangu kwamba sitaweza kufanya mazoezi.

Tuliporudi hotelini akwaambia madaktari kwamba haamini kama kweli ninamajeraha, kwa hiyo wanatakiwa wanipeleke hispitali.

 

“Tulikwenda hospitali na walishuhudia kuwa nilikuwa nina majeraha, wakampelekea kocha ripoti ambayo aliiona yeye mwenyewe. Siku iliyofuata ilikuwa Ramadhani ya mwisho [mfungo wa mwisho kwa Waislamu] niliamka asubuhi nikiwa nimechoka kidogo na kuhisi msuli umekaza kwa hiyo sikwenda pamoja na wenzangu kwenye uwanja wa mazoezi.” – aliendelea Lamine.

“Baada ya mazoezi nilikutana na meneja wa timu akanieleza kwamba kocha anahitaji kikao cha pamoja na sisi, nikamwambia sawa nikaamua kufanya haraka kwenda kuswali kabla ya kikao kuanza.

Niliporudi sikukuta mtu yeyote sehemu ambapo tulikubaliana kikao kingefanyika, nikarudi chumbani kwangu. Saa mbili baadaye, meneja wa timu akanipigia kunijulisha kwamba uongozi umesema natakiwa nirudi Dar es Salaam. Sikusema chochote nikaondoka Mtwara lakini nilikutana na Engineer uwanja wa ndege wakati naondoka.

Baadaye nikaona Bumbuli amepost Instagram kwamba sina nidhamu nilipigana na kocha na ameniamuru nirudi nyumbani [Dar]. Nikampigia simu Engineer na Dr. Msolla mara kadhaa lakini wote hawakupokea simu zangu.

Nilimtumia ujumbe Dr. Msolla akasoma lakini hakunijibu chochote, nikaamua kukaa kimya. Hakuna aliyenipigia tangu siku hiyo hadi Kaimu Katibu Mkuu aliponipigia leo [Mei 27] kwamba wananihitaji ofisini.” aliongeza Lamine.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa