Kocha Frank Lampard akimzungumzia Olivier Giroud;
“Ilikuwa ni usiku wa kiwango chake kizuri na anastahili kupata pongezi kwa kazi kubwa aliyoifanya. Kufunga magoli manne kwenye hatua hii ni jambo la kuvutia, lakini kwa aina ya magoli aliyofunga ni jambo kubwa pia.”

“Nimevutiwa na jinsi alivyokuwa bora lakini pia nimevutiwa na jinsi timu ilivyokuja mpaka Sevilla, mahali ambapo kwa hakika sio mahali parahisi, lakini wamekuja na kucheza kwa kiwango chao chote, ni jambo zuri.”

“Ilikuwa mechi nzuri ambayo timu imepambana kwa kila hali, Giroud anastahili pongezi zote kwa kiwango kizuri alichokionyesha.”

Giroud, Lampard Akiri Giroud wa Moto, Meridianbet

“Giroud ni aina ya mchezaji anayeweza kukupa vitu vingi uwanjani, anaweza kufunga kwenye michuano mikubwa kama hii, anaweza kufunga akiwa na timu ya taifa na bila shaka rekodi yake ya ufungaji inaonyesha kwa kiasi gani alivyobora. Ni takwimu nzuri pia kufunga magoli mengi zaidi ya Zidane, lakini kwangu hilo silizingatii sana. Nazingatia zaidi ule mchango alionao kwa Chelsea ndani na nje ya uwanja.”

“Hakuna mchezaji mwenzake ambaye hajafurahishwa na aina ya kiwango alichokionyesha Giroud kwasababu mwenyewe ni mtu wa kuwa karibu na kila mchezaji na amekuwa akijumuika vyema kwenye mazoezi. Magoli manne kwa nafasi yake na aina ya ngazi tuliopo kwasasa, ni jambo kubwa.”

“Na bila shaka ameleta ushawishi wa kuanza kwenye mchezo ujao (vs Leeds united). Hakuna cha zaidi angeweza kufanya usiku wa leo ili kushawishi aweze kuanza. Ila tutaangalia itakuwaje baada ya mchezo wa leo, lakini magoli manne, ni ngumu kukataa kwamba ameleta ushawishi mkubwa. Sio kuhusu magoli yake tu, ila kiwango kwenye mchezo mzima alikuwa bora sana.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Giroud, Lampard Akiri Giroud wa Moto, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

22 MAONI

  1. Hakuna shaka Giroud ni bora kuliko Tammy Abraham ambaye amecheza mechi nyingi lkn hajafunga magoli kama mshambuliaji tegemeo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa