Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard amesema anajua kua klabu ya Everton inahitaji kupata matokeo ya ushindi lakini yeye hahitaji kuhakikishiwa kuendelea kuwepo kazini.

Baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa Brighton siku ya jumanne cha magoli manne kwa moja kimefanya klabu hiyo kushuka chini na kufika kwenye timu tatu za mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Jambo ambalo linamuweka kocha huyo kwenye wakati mgumu.lampardKocha Lampard ambaye alitangazwa kuchukua nafasi ya kocha Rafa Benitez mwezi Januari mwaka 2022, Amefanikiwa kushinda michezo tisa pekee kwenye michezo 36 ambayo ameisimamia klabu hiyo kutoka jiji la Liverpool.

Kocha huyo alifanikiwa kuiepusha klabu ya Everton kushuka daraja msimu uliomalizika baada ya kupata matokeo ya ushindi katika michezo ya mwisho ya ligi hiyo, Ikielezwa kua ndio sababu ya klabu hiyo kumuacha kocha huyo mpaka sasa licha ya matokeo mabaya ambayo klabu hiyo inaendelea kuvuna.lampardKocha Frank Lampard ameeleza yeye yupo kuhakikisha kua timu hiyo inafanya vizuri na kushinda michezo ambayo ipo mbele yao, Lakini hahitaji kuhakikishiwa usalama wa ajira yake siku za mbeleni na lengo lake kubwa ni kuhakikisha klabu hiyo inabaki kwenye ligi kuu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa