Miongoni mwa majina yanayotajwa kurithi mikoba ya Roy Hodgson pale Crystal Palace, lipo jina la Frank Lampard, kocha wa zamani wa Chelsea ambaye hakuwa na wakati mzuri sana kutumia leseni yake ya ukocha kwa mara ya kwanza klabuni hapo.

Lampard anaweza kupata kazi hiyo endapo tu, Crystal Palace wataamua kumuacha kocha wao Roy Hodgson aondoke klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika.

Kutoka kwenye jarida la the Telegraph orodha ya majina yaliyotolewa jina la Lampard limeonekana kupewa kipaumbele kuchukua nafasi hiyo. Japo kuna majina mengine kama kocha wa Burnley Sean Dyche na kocha wa zamani wa Bournemouth, Eddie Howe, ambaye anahusishwa kujiunga na Celtic kwa muda sasa.

Endapo Lampard atafanikiwa kuchukua mikoba pale Crystal Palace, basi anaweza kufanya sajili kadhaa kuimarisha kikosi chake. Miongoni mwa wachezaji hao ni Tammy Abraham ambaye anatarajiwa kuondoka klabuni hapo majira ya joto.

Bado ulimwengu unakumbuka kuwa Frank alikalia kiti cha kocha wa Chelsea kwa muda wa miezi 18 tu! huku akiweka rekodi mbaya sana. Ambapo aliongoza michezo 84, akishinda 44, kudroo 17 na kupoteza 23!


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Lampard, Lampard Kumrithi Hudgson Crystal Palace?, Meridianbet

CHEZA HAPA

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa