Huenda maisha ya Kepa Arrizabalaga yakaendelea kuwa magumu zaidi ndani ya kikosi cha Chelsea. Hii ni baada ya Frank Lampard kunukuliwa akisema Mendy ndio kipa namba 1 wa Chelsea kwa sasa.

Baada ya Kepa kuonesha kiwango duni, kocha aliingia sokoni kutafuta mbadala na kuinasa saini ya Edouard Mendy ni kama ametua mzigo mkubwa mabegani mwake.

Katika mchezo dhidi ya Sevilla kunako Ligi ya Mabingwa – UEFA, Mendy alionesha kiwango thabiti akihakikisha Chelsea hawaruhusu goli na mchezo kumalizika kwa sare ya 0-0, kiwango cha Mendy kilimkosha Lampard.

“Kwa namna alivyocheza mechi 3 tangu ajiunge nasi, amecheza vizuri sana. Hivyo, kwa sasa ni kipa namba 1.

“Wakati anakuja nilisema ni vizuri kwasababu ya ushindani. Tuliujua ubora wake na sasa anauonesha kila mara. Lakini hicho ni kitu ambacho yeyote anaweza kukipata muda wowote, hiyo ndio maana ya ushindani katika timu. Ninafurahia kwa namna anavyocheza.” alisema Lampard.

Hii ilikuja baada ya Lampard kuulizwa kama Mendy ndio anachukua nafasi ya kipa namba 1 kwenye kikosi chake baada ya Kepa ambaye ni kipa ghali zaidi duniani kuonesha kiwango kibovu kwa muda sasa.


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

35 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa