Ilikuwa ni wakati mgumu sana ambao kocha huyo aliweza kuipokea timu hiyo ambayo wengi walidhania ni kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa inaelekea kuwa na msimu mgumu sana katika soka baada ya kukutana na changamoto kubwa kutokana na kuvunja baadhi ya kanuni ambazo zimewekwa ndani ya soka.
Kuna taarifa hata ndani ya klabu hiyo zilionesha kwamba hata mmiliki wa klabu hiyo alikuwa amefikira tayari kuiuza klabu hiyo kwa sababu hakuwa tayari kuendelea kuingia hasara za kiuendeshaji lakini baada ya kuwasili kwa nyota huyo wa zamani aliweza kurejesha heshima ya klabu hiyo mapema sana kabla mambo hayajabadilika.
Lakini hadi sasa anaonekana kuibua maisha mapya ya kikosi hicho kwa sababu ameweza kukirejesha kwenye ushindani kwa kutumia nyota walewale aliokuwa nao kuweza kusonga mbele zaidi hata kwenye ligi kuu ya nchini humo. Jambo ambalo limeonesha mafanikio makubwa sana kwake.
Mbali na hilo klabu ilikutana na changamoto mbalimbali ambazo hazikumtisha Lampard kuipokea klabu hiyo na kuanza kuijenga kwa kutumia idadi ya nyota alio nao kikosini hapo hadi akafanikiwa kuweza kusonga mbele kwenye michuano ya klabu bingwa jambo ambalo halikufikiriwa kabisa.
Kwa sasa yupo katika nafasi nzuri huku akiwa na faida kubwa baada ya kufutiwa sharti lao walilokuwa wamewekewa la kuzuiliwa kufanya usajili kikosini hapo. Jambo hilo litasaidia nyota huyo kuchagua idadi ya nyota atakaowataka waweze kuongeza kitu ndani ya kikosi chake hicho.
Kwa wakati uliopo ana nafasi kubwa ya kufanya vyema kwenye michuano inayofuata baada ya dirisha la Januari kufunguliwa. Kocha huyo ameweza kuweka utani kidogo kutokana na nafasi ya kusajili aliyopewa kwa kusema kuwa anaitaka klabu hiyo isajili miamba wa soka watatu duniani yaani Messi, Ronaldo na Mbappe.
Japo alilisema hilo katika hali ya utani akiwa na imani kwamba kwa sasa milango ya mafanikio ndani ya klabu hiyo imefunguka na anaweza kufanya analotaka sokoni kutokana na uhitaji ambao kama klabu watahitaji ili kuweza kuziba nafasi na kuleta ushindani zaidi katika nafasi walizopo.
Povel
Habar njema