Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameweka wazi kua hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Uholanzi anayekipiga ndani ya klabu hiyo Frenkie De Jong.
Rais Laporta amesema walipokea ofa ya Euro milioni 100 kwajili ya kiungo Frenkie De Jong, Lakini kama klabu hawakutaka kupokea kiasi hicho cha pesa kwakua wanamuhitaji mchezaji huyo klabuni hapo na ni mchezaji wao muhimu.Kiungo Frenkie De Jong amekua mchezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha Barcelona chini ya kocha Xavi, Ikiwa ni mapinduzi ambayo ameyafanya kiungo huyo vaada ya mwanzo kuonekana hakua chaguo la kwanza la kocha Xavi.
Rais Laporta amekua akieleza mara nyingi kua kuna vilabu vilituma ofa kubwa kwajili ya kiungo huyo, Lakini ni ngumu kwao kumuachia mchezaji ambaye ni muhimu kwenye timu yao.Kiungo De Jong alikua anafukuziwa kwa karibu sana na klabu ya Manchesre United tangu dirisha kubwa lililopita, Lakini kiungo huyo mwenyewe aliweka wazi matamanio yake ambayo ni kukipiga ndani ya klabu ya Barcelona na hana mpango wa kutimka.