Laporta: Mtu wa Ndoto Kubwa, Itawezekana?

Joan Laporta ni miongoni mwa majina yenye heshima kubwa kwenye historia ya FC Barcelona. Aliiongoza timu hiyo kisha akaachia ngazi na akachaguliwa tena kurejea kwenye uongozi kama raisi wa klabu hiyo.

Laporta ameichukua mikoba ya Barca kutoka kwa Bartomeu ambaye alijiuzulu kutokana na sababu nyingi ikiwemo sakata la Messi kutaka kuondoka klabuni hapo, madeni makubwa yanayoikabili klabu na mambo mengine mengi.

Kwa wanaomfahamu Joan, wanaweza kumuelezea vizuri kama ni mtu wa ndoto kubwa. Haijalishi ndoto yake inauhalisia kiasi gani, anaamini lolote linawezekana. Muda ndio kitu cha msingi zaidi.

Baada ya kushinda kiti cha Uraisi wa Barca, Laporta aliweka wazi adhma yake ya kumshawishi Messi kusalia Camp Nou, katika hili ni kama amefanikiwa kutokana na taarifa kuwa nahodha wa klabu hiyo anaweza kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki klabuni hapo.

Licha ya uhalisia kuwa Messi anamapendekezo ya usajili kutoka kwenye vilabu mbalimbali ambavyo kimsingi vinamlipa zaidi ya mshahara wake wa Barca, nyota huyu wa dunia inasemekana amependezwa na uwepo wa Joan na hivyo anatazamia kubaki kwenye klabu aliyoitumikia tangu akiwa mtoto.

Kubaki kwa Messi ni ushindi kwa Laporta, lakini ushindi huu unaongezwa chachu na ndoto kubwa ya kutaka kumuweka Cristiano Ronaldo kwenye timu moja na Lionel Messi. Naam! Mafahali wawili ndani ya zizi moja, itawezekana?

CR7 amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Juventus, kumsajili inaweza isiwe shida lakini suala la mshahara wake ikilinganishwa na hali ya kiuchumi ya FC Barcelona, hili litawezekana? Joan anakwambia kila kitu ni mipango, kwa mpango wa Barca, wanafikiria kuwapeleka wachezaji watatu Juventus na mshahara wa wachezaji hawa utakuwa ni sehemu ya mshahara wa CR7 kama ndoto ya Joan itatimia kuelekea msimu ujao.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe