Laporte Ajiunga Rasmi Al-Nassr

Beki wa kimataifa wa Hispania ambaye alikua anaitumikia klabu ya Manchester City Aymeric Laporte amefanikiwa kujiunga na klabu ya Al-Nassr inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia.

Beki Aymeric Laporte amekua ndani ya Manchester City kwa takribani miaka minne, Lakini mabingwa wa kombe la Arabs walifanikiwa kugonga hodi Man City na kuhitaji huduma ya beki huyo na kufanikiwa kupata saini yake.laporteManchester City wamepokea kiasi cha Euro milioni 30 kutoka kwa Al-Nassr na kuamua kumuachia beki huyo kutokana na kuridhishwa na kiwango cha pesa ambacho kimetolewa na klabu ya Al-Nassr.

Beki huyo ambaye alikua moja ya wachezaji muhimu ndani ya Manchester City wakati akihudumu klabuni hapo kwa miaka minne aliyokaa hapo, Lakini ameamua kwenda Uarabuni kwajili ya kupata changamoto nyingine.laporteKitasa Aymeric Laporte anaungana na wachezaji wengine wengi waliotoka ligi mbalimbali barani ulaya na kuelekea nchini Saudia Arabia, Lakini pia beki huyo atakumbukwa klabuni hapo kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye timu hiyo ikiwemo msimu wa mwisho ambao wametwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja.

 

Acha ujumbe