Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino amesema kua kiungo wa klabu hiyo Romeo Lavia ameshapona na ameanza mazoezi na wachezaji wenzake.

Kiungo Romeo Lavia amekua na majeraha tangu atue klabuni hapo na kushindwa kupata nafasi ya kuitumikia timu hiyo, Lakini kocha wake ameeleza yuko mbioni kuanza kuitumikia timu hiyo.laviaKocha Pochettino wakati akifanya mahojiano na wanahabari leo ameeleza kua kiungo raia wa kimataifa wa Ubelgiji ameanza mazoezi, Hivo kuanzia wiki ijayo atajummuishwa kwenye timu ili aweze kuisaidia klabu hiyo katika michezo yake.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Southampton ambaye tangu ajiunge na matajiri hao kutoka jiji la London hajafanikiwa kucheza mchezo hata mmoja kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama.laviaRomeo Lavia inaelezwa baada ya mapumziko ya kimataifa anaweza kuanza kuitumikia klabu hiyo, Huku mashabiki wa klabu ya Chelsea wakiwa na hamu kubwa ya kumuona mchezaji huyo dimbani akiipigania jezi ya klabu yao pendwa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa