Lazio na Napoli wote wameonyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Florian Neuhaus Januari.
Vilabu vyote viwili vina nia ya kuimarisha safu zao za kati mwezi huu huku wakipania kusalia katika kinyang’anyiro cha kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. Biancocelesti wamefanya vyema zaidi kuliko mabingwa hao watetezi katika wiki za hivi karibuni na kukaa pointi tatu nyuma ya Fiorentina walioshika nafasi ya nne.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Neuhaus ameanza kushuka kiwango katika Borussia Monchengladbach msimu huu, akianza mara moja tu katika mechi nane zilizopita za Bundesliga. Ana kandarasi na klabu hiyo ya Ujerumani hadi Juni 2027.
Kama ilivyoripotiwa na Di Marzio, Lazio na Napoli wote wamewasiliana na Monchengladbach kuomba taarifa kuhusu mkataba wa mkopo na chaguo la kununua kwa Neuhaus.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 amecheza kwa dakika 697 katika mechi 16 kwa upande wa Bundesliga msimu huu, akifunga mabao matatu na kutoa asisti mbili kwa wakati huo.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Napoli pia wamekuwa wakihusishwa na kutaka kumnunua kipa wa Udinese Lazar Samardzic lakini sasa wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Brighton wa Roberto De Zerbi.