Leicester City Yampa Kazi Van Nistelrooy

Klabu ya Leicester City ambayo imemfuta kazi aliyekua kocha wake Steve Cooper sasa wamemuajiri aliyekua kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United Ruud Van Nistelrooy raia wa kimataifa wa Uholanzi.

Leicester City wamefanya mazungmzo na kocha Van Nistelrooy wiki hii baada ya kumfuta kazi Steve Cooper ambapo mazungumzo yao yalienda vizuri na kupelekea kocha huyo kukubali kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ambayo haipo kwenye kipindi kizuri sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza.leicester cityKocha Ruud Van Nistelrooy ambaye aliiongoza klabu ya Manchester United kwa michezo minne baada ya Erik Ten Hag kufukuzwa kazi na kufanikiwa kushinda michezo mitatu na kusuluhu mchezo mmoja, Hali iliyowafanya mashabiki wa Man United kutamani kumuona akiendelea kua sehemu ya timu hiyo.

Baada ya kocha Ruben Amorim kutangazwa kama kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Van Nistelrooy alitimka klabuni hapo, Lakini Leicester City wameonekana kumuamini na kuona ndio kocha sahihi kwasasa kuivusha klabu yao na kuamua kumpa timu na sasa ni muda wa gwiji huyo kuonesha ubora ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa Uingereza mwaka 2016.

Acha ujumbe