Leny Yoro Apata Majeraha

Beki mpya wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Leny Yoro (18) amepata majeraha usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Arsenal.

Mchezo huo ambao umepigwa nchini Marekani na Man United kupoteza kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Arsenal uliwaacha United na masikitiko, Kwani mchezaji wao Leny Yoro hakufanikiwa kumaliza mchezo ambapo alitoka baada ya dakika 32 tu za mchezo kuashiria alipata majeraha.yoroKitendo cha beki huyo kupata majeraha inaendelea kuleta ishara mbaya kwa Man United kabla ya msimu kuanza kwani msimu uliomalizika klabu hiyo ilikua moja ya vilabu vilivyoandamwa na majeraha sana, Huku msimu huu hali ikionekana kuanza mapema kabla hata ya msimu kuanza rasmi.

Kocha Ten Hag amesema mpaka sasa hawajajua tatizo litakua kubwa kiasi gani kwa beki Leny Yoro lakini wanapswa kusubiri kwa masaa 24 ili kujua majeraha hayo yatakua makubwa kwa kiasi gani, Kwasasa jopo la madaktari wa klabu hiyo lipo kwenye uchunguzi wa kutambua jeraha hilo ni kubwa kiasi gani na anaweza kukaa nje kwa muda gani.

Acha ujumbe