Leny Yoro Mazoezini Carrington leo

Beki mpya wa klabu ya Manchester United mwenye umri wa miaka (18) Leny Yoro ambaye amesajiliwa kutoka klabu ya Lille ya nchini Ufaransa amefanikiwa kufanya mazoezi na kikosi cha timu hiyo leo.

Leny Yoro ametambulishwa rasmi jana ndani ya klabu hiyo lakini leo ameweza kuhudhuria mazoezi ya klabu hiyo katika kiwanja cha mazoezi ya klabu hiyo kinachofahamika kama Carrington, Hii inaonesha kwa kiwango gani mchezaji huyo ana njaa kushinda ndani ya klabu hiyo.leny yoroBeki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa inaelezwa anaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Rangers kutoka nchini Scotland, Mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kesho kabla ya kusafiri kwenda nchini Marekani.

Klabu ya Manchester United baada ya mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya Rangers inatarajiwa kwenda kufanya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani ambapo itacheza michezo kadhaa ya kirafiki, Huku beki Leny Yoro nae akitarajiwa kua sehemu ya kikosi ambacho kitasafiri kuelekea Marekani.

Acha ujumbe