Leny Yoro na Man United Mambo Safi

Baada ya upinzani mkali na majadiliano ya muda mrefu hatimae klabu ya Manchester United iko mbioni kukamilisha dili la beki kinda mwenye uwezo mkubwa Leny Yoro (18) kutokea Lille ya Ufaransa.

Manchester United ilikua inakumbana na upinzani mkali kwenye dili hilo kutoka kwa mabingwa wa ulaya klabu ya Real Madrid ambayo ilikua ikielezwa ndio kipaumbele cha mchezaji mwenyewe, Lakini mapema leo taarifa zimetoka kua mchezaji huyo amekubali kujiunga na klabu ya Man United.leny yoroManchester United walituma ofa ya Euro milioni 50 kwa klabu ya Lille ambayo ndio inammiliki mchezaji Leny Yoro wiki kadhaa zilizopita na ofa yao kukubaliwa. Lakini changamoto ilikua upande wa mchezaji ambaye ilielezwa kwa kiwnago kikubwa alikua anaisubiri klabu ya Real Madrid.

Baada ya mazungumzo ya kina kutoka jana hatimae beki huyo amekubali kujiunga na Man United kutokana na kile kilichoelezwa ushawishi mkubwa klabu hiyo, Lakini pia klabu ya Lille imesukuma sana dili hilo kutokea kwakua hawakutaka kumpoteza kijana huyo bure kwakua mkataba wake ulikua umebaki mwaka mmoja.leny yoroTaarifa kutoka nchini Ufaransa zinaeleza Leny Yoro amesafiri kuelekea jijini Manchester kwajili ya kufanya vipimo vya afya ili kukamilisha dili lake la kujiunga na Man United, Huku mashetani wekundu wakielezwa wanataka kukamilisha dili hilo haraka zaidi ili kuepuka kuvurugika au kuingiliwa na timu yeyote.

Acha ujumbe