Baada ya Neymar kutamka hadharani uwezekano wa kucheza na Messi mwakani, Mkurugenzi wa michezo wa PSG – Leonardo Araujo, akwepa kuzungumzia hilo.

Wiki iliyopita, Neymar alisikika akisema anataka kucheza na Messi mwakani. Hii ni kauli iliibua hisia na hali ya sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa PSG na Barcelona.

Swali ni Je, Messi atakwenda PSG au ni Neymar Jr anarudi Barcelona? Leonardo anatupa jibu kwa upande wa PSG.

Leonardo Araujo, Leonardo Araujo Amekwepa Usajili wa Messi., Meridianbet
Lionel Messi (kushoto) walipokuwa na Neymar Jr (kulia) ndani ya Barcelona.

Akizungumza na Canal+, Leonardo Araujo amesema ” unajua, ni kitu cha kawaida kwa Neymar kumwambia vile mwandishi wa Argentina. Alipaswa kumzungumzia Messi, ni kawaida.

“Tunapaswa kuendelea kuwaheshimu wengine. [Messi] ni mchezaji wa Barcelona. Inapotokea mtu anawaongelea wachezaji wetu, hatufurahishwi.

“Kwahiyo hatuwagusi wachezaji wa watu wengine. Huu sio muda wa kuangalia dirisha la usajili. Tunafuraha na kikosi tulichonacho, tunafikiria zaidi msimu huu na hasa kipindi hiki cha kwanza cha msimu ambacho kimekuwa kigumu sana.

“Tunapaswa kuyaangalia zaidi malengo yetu ikiwa ni pamoja na kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa. Pia tunatakiwa kuiwaza Ligue 1 na kuzuia kuingia kwenye wakati mgumu, tuzingatie hayo”.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

Leonardo Araujo, Leonardo Araujo Amekwepa Usajili wa Messi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

24 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa