Barcelona walipata ushindi wao wa kwanza msimu huu kwenye La Liga, kwa kuwalaza Real Sociedad 4-1 Jumapili usiku, huku Robert Lewandowski akifunga mabao yake ya kwanza kwa klabu hiyo.

lewandowski, Lewandowski Aendeleza Ubabe wake Barcelona., Meridianbet

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland alifunga goli lake la kwanza sekunde 43 tu kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Alexander Isak. Ousmane Dembele alirejesha uongozi wa Barca kabla ya Lewandowski kufunga bao la pili na Ansu Fati akakamilisha kipigo hicho.

lewandowski, Lewandowski Aendeleza Ubabe wake Barcelona., Meridianbet

Ndiyo kusema kwamba Barca Gari limewaka?

Ilikuwa ni sare ya 0-0 ya kusikitisha na ya kukatisha tamaa na Rayo Vallecano wiki iliyopita lakini Barcelona walikuwa katika kiwango bora zaidi kipindi cha pili huko San Sebastian, waliuwasha sana moto kwa wapinzani wao ambao hawakuweza kumudu ubora wao huku Lewandowski na Fati wakiudhibiti mchezo na kufanikisha Barca kupata pointi tatu.

lewandowski, Lewandowski Aendeleza Ubabe wake Barcelona., Meridianbet

Imekuwa ni misimu kadhaa migumu kwa Barcelona, ​​mambo hayakwenda sawa chini ya Ronald Koeman, walimpoteza Lionel Messi na kwa masuala ya fedha kila kitu kilianza kuyumba.

lewandowski, Lewandowski Aendeleza Ubabe wake Barcelona., Meridianbet

Lakini, Xavi sasa ndiye msimamizi na ametumia gharama za kawaida tu msimu huu wa joto. Robert Lewandowski bila shaka atakuwa shujaa wa Barca kwa kufunga mabao mengi zaidi ukiwajumuisha na Pedri, Fati na Gavi Barca wanaweza kushindania ubingwa. Wana nguvu za kina pia, wachezaji wapya waliosajiliwa Raphinha alikuwa kwenye benchi na Jules Kounde bado hayupo. Kuikamata Real Madrid huenda ikawa ngumu lakini kama watacheza kwa kiwango kama kile cha kipindi cha pili watakuwa na nafasi ya kuwafikia Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa