Klabu ya Barcelona imembadilishia namba mchezaji wake mpya aliyesajiriwa akitokea Bayern Munich Robert Lewandowski kutoka namba 21 ambayo alikuwa anavaa kwenye michezo ya Pre-seaosn na kupewa jersey namba 9.

Jersy namba 9 msimu uliopita ilikuwa inavaliwa na mchezaji wa kimataifa kutoka Uholanzi Memphis Depay kwenye klabu hiyo, huku Lewandwski akiwe kwenye klabu ya Bayern alikuwa akivaa namba hiyo, ila baada ya kusajiriwa na klabu ya Barcelona alikabidhiwa Jersey namba 21 ambayo aliivaa kwenye michezo ya Pre-season.

Lewandowski, Lewandowski Kuvaa Namba 9, Meridianbet

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta alipoulizwa swala hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari, aliweka sawa kuwa swala kubadirishana namba halikuwa makubaliano ya wachezaji bali yalikuwa maamuzi ya klabu.

“Yalikuwa maamuzi ya klabu. Kwa sababu ya manufaa ya klabu, muinekano, matangazo. Tulidhani yalikuwa maamuzi sahihi.  Tukufanya kwa heshima kubwa kwa Mephid, ambaye anaelewa vizuri.” Alisema Laporta.

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa