LIGI KUU ITAANZA NA SURA HII HAPA

BURUDANI ya Ligi Kuu Bara ipo njiani kurejea baada ya ratiba ya mechi za ufunguzi kutolewa hivyo ni muda wa kila mmoja kutambua kipi ambacho atavuna kwa msimu mpya wa 2024/25.

Ni Agosti 8 2024 ambapo wababe wawili Simba na Yanga watakutana hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba Simba walitwaa taji hilo msimu wa 2023/24 kwenye fainali walipokutana na Yanga kwa ushindi wa penalti, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 16 inawakutanisha washindi wa nafasi nne za juu kwenye ligi.

Ni Yanga iligotea nafasi ya kwanza, Azam FC nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu na Coastal Union nafasi ya nne kwenye msimamo msimu wa 2023/24.

Azam FC itamenyana na Coastal Union Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba Uwanja wa Mkapa na mchezo wa mshindi wa tatu na fainali itachezwa Agosti 11, Uwanja wa Mkapa.

Acha ujumbe