Ligue 1 Ufaransa Imeisha Rasmi!

Msimu wa Ligi 2019/20 wa Ligue 1 na Ligue 2 umeisha rasmi! Tofauti na nchi zingine ambazo bado zinajaribu kutafuta namna bora ya ya kuendeleza ligi kwa baadhi ya mechi ambazo zimesalia kwenye ligi kuu, ufaransa kwao hili limekuwa tofauti baada ya Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe kutangaza kumalizika kwa msimu.

Virusi vya corona vimesababisha kusimama kwa ligi nyingi duniani huku tangia mapema mwezi Machi, huku nchi nyingi zikiwa na sera ya kutotoka nje na kukaa ndani mpaka pale hali itakapo kaa sawa.

Uamuzi wa Ufaransa unawafanya waungane na nchi zingine za Netherlands, Belgium na Argentina ambao wameamua kutangaza kuisha kwa msimu wa soka wa 2019/20, kwa kuwa hawana mpango wa kujaribu kuendeleza ligi hata baada ya msimu wa joto.

“Msimu huu hauwezi kuendelea, hakutakuwa na matukio makubwa ya michezo, hasa soka kabla ya septemba, hata bila kuwa na mashabiki.” -Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe

Hata hivyo, hii inaenda kuwa changamoto kwa vilabua ambavyo bado vipo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

3 Komentara

    Wangesubili msimu umalizike

    Jibu

    Maamuzi mazuri

    Jibu

    Gud news

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.