Lille Yapandisha Yafika €17 Milioni Kwa Zechiël

Klabu ya Lille OSC ya Ufaransa imeongeza presha katika harakati zake za kumsajili kiungo wa Feyenoord, Gjivai Zechiël, baada ya kuwasilisha ofa mpya yenye thamani ya hadi euro milioni 17, ikiwa ni pamoja na bonasi. Lille tayari ilikuwa imeonyesha nia ya kumchukua nyota huyo kwa ofa ya takribani euro milioni 10, lakini sasa imeamua kuongeza dau baada ya kupata fedha nyingi kupitia mauzo makubwa ya Ayoub Bouaddi kwenda Manchester City. Hatua hiyo imefanya vita ya kumsaka Zechiël kuwa moja ya stori zinazotikisa dirisha la usajili.

Lille Yapandisha Yafika €17 Milioni Kwa Zechiël

Bouaddi mwenye umri wa miaka 18 ameuzwa na Lille kwa ada ya msingi ya euro milioni 95, dili lililoweka mazingira mazuri kwa klabu hiyo ya Ufaransa kuendelea kufanya usajili mkubwa. Kwa mujibu wa Dennis Kranenburg wa Rijnmond Sport, Lille sasa imeongeza nguvu katika mazungumzo ya Zechiël na imekuwa ikigonga mlango wa Feyenoord kwa nguvu zaidi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kinachovutia zaidi ni kwamba thamani ya Zechiël kwenye Transfermarket bado inaelezwa kuwa karibu euro milioni 10, lakini Lille sasa ipo tayari kulipa hadi euro milioni 17 kwa jumla kupitia ada na bonasi. Hata hivyo, kiasi hicho huenda kisitoshe kuufanya uongozi wa Feyenoord kubadili msimamo wake. Klabu hiyo inamtazama Zechiël kama mmoja wa wachezaji muhimu zaidi kuelekea msimu ujao na inapendelea kumuweka katika kikosi badala ya kumruhusu kuondoka kwa urahisi.

Lille Yapandisha Yafika €17 Milioni Kwa Zechiël

Kranenburg anaamini swali kubwa ni kama Feyenoord itaendelea kusimamia msimamo wake wa kutomuuza mchezaji anayechukuliwa kuwa muhimu, au kama Lille itafika na kiasi ambacho hakiwezi kukataliwa. “Swali ni kama Feyenoord itachagua kutomruhusu mchezaji wake muhimu, ambaye huenda hata akawa bora zaidi kwa sasa, kuondoka, au kama itakuja ofa ambayo hawawezi kuikataa,” alisema.

Lille Yapandisha Yafika €17 Milioni Kwa Zechiël

Wakati huo huo, Feyenoord inahitaji kuchukua hatua nyingine muhimu ikiwa kweli inataka kumzuia Zechiël, kwanza ni kuboresha na kuongeza mkataba wake. Mkataba wa sasa wa kiungo huyo unaendelea hadi mwaka 2028, lakini kuvutia kwake sokoni kunaweza kuongeza presha ya mazungumzo mapya. Changamoto kubwa ni kama Feyenoord itaweza kushindana na mishahara ambayo klabu kama Lille inaweza kutoa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.