Lingard Awavutia Madrid, PSG na Inter.


 

Jesse Lingard anaripotiwa kufuatiliwa na vilabu vingi vya juu barani Ulaya zikiwemo Real Madrid, PSG na Inter Milan wakati wa mbio kali za top 4 akiwa na West Ham baada ya kuonyesha kiwango bora.

Mchezaji huyo wa miaka 28, aliyejiunga na Wagonga Nyundo kwa mkopo kutoka Manchester United mnamo Januari, amefunga mabao nane katika michezo tisa na kupata kuitwa kwenye kikosi cha England mwezi uliopita.

 

Lingard akishangilia moja ya goli lake wikiendi hii.

Aliendelea kuwa na kiwango kizuri Jumapili pia, akifunga mara mbili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Leicester, na sasa ESPN inaripoti kwamba watatu miongoni mwa vigogo wa Europa wanaangalia mienendo ya Lingard kuelekea kwenye dirisha la msimu wa joto.

Ripoti hiyo inaelezea kuwa West Ham wanataka kumsaini Lingard kabisa na kesi yao itaimarishwa ikiwa wataweza kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Kwa sasa wako nafasi ya nne kwenye msimamo, alama moja mbele ya Chelsea na mbili mbele ya Liverpool wakiwa wamebakiza michezo saba.

Lingard amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa Manchester United na alikuwa hana namba chini ya Ole Gunnar Solskjaer mapema msimu huu.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Jesse Lingard yuko vizuri

    Jibu

    Hata mie ananivutia sana

    Jibu

Acha ujumbe