Lingard Bado Hajaamua Hatma Yake United!

Jesse Lingard anaripotiwa kuwa bado hana uhakika kama anataka kusalia Manchester United kwa msimu ujao 2021-22 au lah atafute klabu nyingine, kwa mujibu wa ripoti.

Nyota huyu Muingereza alikuwa anakosa mda wa kutosha wa kucheza akiwa na Manchester United chini ya Ole Gunnar kwenye nusu ya kwanza ya msimu huu, lakini akaweza kujiboresha na kufanya vyema akitumikia mkopo na West Ham United.

Jesse Lingard
Jesse Lingard

Lingard amechangia magoli 8 na asisti 49 kwenye mechi alizocheza za Ligi ya Primia dhidi akiwa na West Ham. Na vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo vinasema kuwa wapo tayari kufanya kila wawezalo ili kumsaini staa huyu kwa mkataba wa kudumu.

Hata hivyo kwa mujibu wa Goal, staa huyu bado hajafanya maamuzi ni klabu gani anataka kuwepo msimu ujao, na ikiwa atarejea Old Trafford atahitaji kuongezewa mechi zaidi ili mambo yasiwe kama ilivyokuwa awali.

United pia wameripotiwa kuwa wanavutiwa na Declan Rice na wanahitaji kufanya mpango wa kufanya dili la mabadilishano ya wachezaji litakalomhusisha Lingard.


 

JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Kama alipo apaeleweki atafute klabu nyingine

    Jibu

    Declan Rice aende tu united

    Jibu

    Aamue basi mbona wanatutia presha

    Jibu

Acha ujumbe