Mshambuliaji wa Manchester United Jesse Lingard yupo mbioni kurejea Old Traford baada ya kumaliza mkopo wake kwa wagonga nyundo wa London West Ham United.

Westham United ipo kwenye wakati mgumu wa kumnunua moja kwa moja kutokana na thamani halisi ya nyota huyo inatajwa kufikia paun milion 21.
Lingard mwenye umri wa miaka 28 anataka mkataba wa miaka minne na mshahara usiopungua pauni laki moja kwa wiki kiasi ambacho The Hummers huenda ikawa mlima mrefu kwao licha ya kuwa na hitaji nae.
Lingard amebakiwa na mwaka moja katika mkataba wake na mashetani wekundu ambao ni wazi huenda kurejea kwake Old Traford itakuwa ni sawa na kucheza karata isiyo tabirika.
Nyota huyo ambaye ni zao la United amecheza mechi 3 za msimu huu akiwa na Manchester United kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda West Ham United ambapo katika mechi 13 alizocheza amefunga mabao 9.
Miongoni mwa timu alizocheza kwa mkopo ni hizi hapa:-
2012–2013 → Leicester City alicheza mechi 5 na hakufunga bao hata moja.
2013–2014 → Birmingham City alicheza mechi 13 na kufunga mabao (6)
2014→ Brighton & Hove Albion alicheza mechi 15 na kufunga mabao (3)
2015 → Derby County alicheza mechi 14 nakufunga mabao (2)
2021– → West Ham United akicheza mechi 13 amefunga mabao (9) hadi sasa.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Aende tuu kama nafasi ipo
Maamuzi anayo yeye
Maamuzi ni yake mwenyewe
Mamuzi yake yapo sahii