Lionel Messi Akamilisha Ununuzi wa Klabu ya Eldense Inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Nchini Hispania.

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, amechukua rasmi umiliki wa klabu ya Eldense inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania. Klabu hiyo ilithibitisha kukamilika kwa mchakato huo siku ya Alhamisi, hatua inayowakilisha tukio kubwa katika shughuli za kibiashara za nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 nje ya uwanja.

Lionel Messi Akamilisha Ununuzi wa Klabu ya Eldense Inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Nchini Hispania.

Klabu hiyo yenye makao yake Alicante hapo awali ilikuwa inamilikiwa na kampuni ya uwekezaji ya Colombia, Grupo TH, ambayo pia ina hisa katika klabu mbalimbali nchini Colombia na Uswisi. Makubaliano haya yanakuwa mabadiliko ya tatu ya umiliki wa Eldense ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo, dili hilo bado linasubiri idhini rasmi kutoka Baraza la Kitaifa la Michezo la Hispania (CSD). Baada ya kupata kibali hicho, hatua hiyo itaashiria mwanzo wa kipindi kipya chenye malengo makubwa kwa klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania.

Ununuzi huu una umuhimu mkubwa kwa sababu Eldense ndiyo klabu ya kwanza ya kulipwa nchini Hispania ambayo Messi amewekeza. Ingawa mwanzoni mwa mwaka huu alininunua klabu ya daraja la tano, Cornella, timu hiyo bado inachukuliwa kuwa ya nusu-kitaalamu.

Katika taarifa rasmi iliyothibitisha makubaliano hayo, Eldense ilieleza matumaini makubwa kuhusu mmiliki wao huyo mpya mwenye jina kubwa. Klabu hiyo imeeleza kuwa gwiji huyo wa Argentina anaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko na kukuza maendeleo yao ya baadaye.

“Kuwasili kwa mmoja wa watu muhimu zaidi katika historia ya michezo kwenye soka la kulipwa nchini Hispania, akiwa mmiliki wa CD Eldense, kunaashiria mwanzo wa mradi wa muda mrefu unaolenga kuendeleza klabu katika nyanja za michezo, taasisi na jamii,”Klabu hiyo ilisema.

Lionel Messi Akamilisha Ununuzi wa Klabu ya Eldense Inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Nchini Hispania.

Eldense iliyoanzishwa mwaka 1921, imetumia sehemu kubwa ya historia yake ikicheza nje ya madaraja mawili ya juu ya soka nchini Hispania. Klabu hiyo hucheza mechi zake za nyumbani katika Uwanja wa Estadio Nuevo Pepico Amat wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 5,776, uliopo katika jiji la Elda.

Klabu hiyo ilipanda daraja hadi ligi ya pili mwaka 2023 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1964, lakini ikashuka daraja mwaka 2025 kabla ya kurejea tena katika ligi daraja la pili msimu huu wa kiangazi. Nje ya Hispania, Messi pia anahusika kwa sehemu katika umiliki wa klabu ya Deportivo LSM ya Uruguay pamoja na mchezaji mwenzake wa Inter Miami, Luis Suarez.

Umiliki wa Eldense na Cornella hauonekani kusababisha matatizo ya haraka kutokana na tofauti ya madaraja matatu kati ya klabu hizo. Hata hivyo, iwapo Cornella itapanda kupitia madaraja ya ligi, Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) huenda lisiruhusu klabu zote mbili kushiriki katika ligi moja ikiwa Messi ataendelea kuwa mmiliki mkuu wa klabu hizo.

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.