Lionel Messi Mzee wa Kuchapa Rekodi

Huyu ndiye Lionel Messi nyota wa Barcelona ambaye ameandika rekodi kadhaa kubwa! Sasa, kwa mara nyingine ameandika rekodi ya kuchukua kiatu cha dhahabu kwa mara ya sita toka alipoanza kucheza soka la kulipwa.

Messi amemaliza msimu akiwa na Magoli 36 ya La Liga kwa msimu wa 2018/19. Nyota wa PSG, Kylian Mbappe ndiye mchezaji pekee ambaye angeweza kumfikia Lionel Messi kwa magoli, lakini haikuwa ridhiki yake akimaliza msimu kwa magoli 33, magoli 3 nyuma ya Messi.

Baada ya kupokea tuzo hii, Messi ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji pekee ambaye amewea kutwaa tuzo hii kwa misimu 3 mfululizo. Msimu wa mwaka 2016/17 alimaliza na jumla ya magoli 37, na msimu wa 2017/18 alimaliza kwa idadi ya magoli 34.

Messi Mzee wa Kuchapa Rekodi

Wakati akizungumzia ushindi wake huu Messia amesema kuwa hii haikuwa ni kitu alichotarajia. Alisisitiza kuwa hakuwa anafikiria kuhusu mafanikio binafsi isipokuwa alikuwa anaangazia mafanikio ya timu yake.

Messi anawaongoza Barcelona dhidi ya Valencia kwenye fainali ya Copa del Rey Jumamosi hii.

2 Komentara

    Yuko vizur

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

Acha ujumbe