Lionel Messi Yupo Fit Kuwakabili Uruguay

Lionel Messi alikosa mechi mbili za PSG sababu ya kukabiliwa na majeraha ya goti lakini sasa yupo imara kucheza na timu ya taifa ya Argentina dhidi ya Uruguay katika mechi ya kufuzu kombe la Dunia.

Lionel Messi Yupo Fit Kuwakabili Uruguay

Nahodha huyo wa Albiceleste alikosa michezo dhidi ya RB Leipzig katika Ligi ya Mabingwa na mchezo wa ligi dhidi ya Bordeaux baada ya kupata jeraha kwenye mchezo dhidi ya Lille mwezi Oktoba 29.

Kocha wa Argentina alithibitisha kwamba Messi atakuwa tayari kucheza dhidi ya Uruguay na Brazil wakati huu wa mapumziko wa mechi za kimataifa.

“Leo yupo vizuri, jana alifanya mazoezi na sisi, alikuja akiwa katika hali nzuri alikuwa bora kuliko siku chache zilizopita lakini sasa anapatikana,” Scaloni alithibitisha.

Lakini mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo hakufurahishwa na maamuzi ya Scaloni ya kumuita Messi katika timu ya taifa.

“Kwa sasa Messi amecheza sana katika timu ya taifa kuliko klabu yake.” alisema Leonardo.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe