Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Lisandro Martinez amejitonesha jeraha lake ambalo aliumia mwezi Aprili mwaka huu katika mchezo dhidi ya klabu ya Sevillla.
Taarifa kutoka ndani ya Man United zinaeleza Lisandro Martinez ataendelea kukaa nje ya uwanja kwa muda zaidi, Hii ni kutokana na taarifa ya klabu ya Manchester United juu ya maendeleo ya beki huyo.Beki huyo wa timu ya taifa ya Argentina aljitonesha jeraha lake katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal, Jeraha ambalo limemueka nje ya uwanja takribani mwezi sasa na taarifa inaeleza araendelea kukaa nje ya uwanja.
Klabu ya Manchester United inaandamwa na majeraha kwa kiwango kikubwa kwasasa hasa kwenye eneo lake la ulinzi, Kwani mpaka sasa beki kadhaa wanauguza majeraha yao ikiwemo Wan Bissaka, Luke Shaw, pamoja na Sergio Reguilon.Lisandro Martinez baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mzima sasa, Inaelezwa anaweza kuendelea kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili mpaka tatu zaidi jambo ambalo litaisumbua Man United kwani ni moja ya mchezaji tegemezi kikosini.