Lisandro Martinez Arejea Kiwanjani

Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Lisandro Martinez hatimae ameonekana kurejea kiwanjani baada ya kupata majeraha yaliyomueka nje kwa miezi takribani miwili.

Lisandro Martinez alipata majeraha katika mchezo wa robo fainali kati ya Manchester United dhidi ya Sevilla katika michuano ya Europa League, Hadi kumpelekea beki huyo kufanyiwa upasuaji na kukosa msimu wote uliobakia.lisandro martinezBeki huyo wa kimataifa wa Argentina ameonekana akifanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji huo, Hali ambayo imeonesha kua beki huyo amerejea uwanjani na yuko tyari kuanza maandalizi ya msimu ujao pamoja na wenzake.

Baada ya kuonekana akifanya mazoezi Lisandro Martinez pia aliweka kwenye mtandao wake wa Twitter na kuandika ana furaha ya kurejea imara kwa asilimia 100 na hapa ndipo mashabiki wa klabu hiyo walipopokea taarifa hiyo kwa shangwe kubwa.lisandro martinezKurejea kwa Lisandro Martinez mapema ndani ya kikosi cha Manchester United ni furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo, Lakini pia kwa kocha Erik Ten Hag ambaye atajua namna gani ataanza kukisuka kikosi chake kuelekea msimu ujao huku akiwa na wachezaji wake muhimu.

Acha ujumbe