Lisandro Martinez Kukosekana dhidi ya Ipswich Leo

Beki wa kimataifa wa Argentina anayekipiga ndani ya klabu ya Manchester United Lisandro Martinez inaelezwa atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Ipswich Town.

Lisandro Martinez inaelezwa alikua  na majeraha madogo ambayo yalimfanya akashindwa kujiunga na timu ya taifa ya Argentina, Hivo majeraha hayo yanaonekana bado hayajapona na ndio sababu atakosekana katika mchezo wa leo ugenini dhidi ya klabu ya Ipswich.lisandro martinez

Beki huyo wa kimataifa wa Argentina amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara tangu ajiunge na klabu ya Manchester United akitokea klabu ya Ajax mwaka 2022, Hali hiyo imekua ikiiumiza klabu hiyo kwani beki huyo amekua moja ya wachezaji muhimu klabu hapo hivo kukosekana kwake inakua pengo kubwa.

Beki Lisandro Martinez sasa anaongeza orodha ya majeraha klabuni hapo kufikia wawili kwani mchezaji pekee ambaye alikua hajapona klabuni hapo ni Harry Maguire peke, Kuongezeka kwa beki huyo kunafanya idadi kuongezeka kufikia wawili lakini Man United kwasasa wameonekana kua na machaguo ya kutosha kwenye eneo la ulinzi.

Acha ujumbe