Dau Litawakwamisha United Tena kwa Sancho?

Klabu ya Manchester United inatajwa kuwa tayari ipo kwenye maandalizi ya kuwasilisha ofa ya £80m kwa ajili ya kumsajili nyota wa Borrusia Dortmund, Jadon Sancho katika dirisha la msimu huu wa joto.

Mashetani wekundu walikuwa wanahusishwa kwa ukaribu sana na mshambuliaji huyu msimu uliopita, lakini hawakuwa tayari kulipa dau la £108m lililokuwa linatajwa na Dortmund.

Sancho amekuwa kwenye fomu nzuri sana msimu huu akifunga jumla ya magoli 14 na kutoa usaidizi wa magoli 18 kwenye mechi 35 alizocheza za michuano yote.

Jadon Sancho

Suala la uhamisho wa staa huyu wa zamani wa City linaendelea kushika kasi kwenye vichwa vya habari za michezo, huku klabu za Man United, Chelsea na Liverpool zikitajwa kuwa kwenye kinyang’anyiro cha saini yake.

Kwa mujibu wa Daily Star, United wamejiandaa zaidi kuhakikisha wanaipata saini ya nyota huyu wa miaka 21, na wameandaa fungu la £80m  kwa ajili ya huduma yake.

HGata hivyo, Sancho anaripotiwa kuwa na furaha kwenye klabu yake ya sasa Ujerumani.


Pesa Ipo Hapa Katika Kasino ya Lucky Lucky.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

8 Komentara

  Safi sana kama watampata

  Jibu

  Vizuri sana

  Jibu

  Vizuri

  Jibu

  Good

  Jibu

  Vizuri lazima ugalamie

  Jibu

  Safii

  Jibu

  Sio mchezaji mzur San Ivo tu

  Jibu

  United wanazidiwa

  Jibu

Acha ujumbe