Liverpool Dhidi ya Chelsea Vita inahamia Uwanjani

Leo kitapigwa kipute kati ya klabu ya Liverpool dhidi ya Chelsea ambao watakua nyumbani katika dimba lao la Stamford Bridge katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Liverpool na Chelsea wamekua na vita siku za hivi karibuni nje ya uwanja ambapo vita hiyo imesababishwa na kiungo wa klabu ya Brighton Moises Caicedo ambaye anawaniwa na vilabu vyote viwili, Hivo leo vita hii inatarajiwa kuhamishiwa uwanjani.liverpoolMajogoo hao wa Anfield na Chelsea mara ya mwisho kukutana katika ligi kuu ya Uingereza walitoka sare katika michezo yote miwili,Ambapo timu zote zilikua katika msimu mbaya zaidi kwa upande lakini msimu huu wanatarajiwa kufanya vizuri zaidi.

Vijana wa Jurgen Klopp wanataka kufanya vizuri zaidi msimu huu kwani msimu uliomalizika walikua na msimu mbaya, Ambapo ilipelekea mpaka kukosekana katika ligi ya mabingwa ulaya na kampeni inaanzia darajani leo.liverpoolChelsea wao pia sio wadhaifu japo wapo kwenye mchakato wa kutengeneza timu mpya yenye ushindani chini ya kocha Pochettino, Hivo mchezo huo kati ya Liverpool na Chelsea unatarajiwa kua wenye mvuto na ushindani mkubwa.

Acha ujumbe