Liverpool Dhidi ya Man City Ngoma imelala Kati

Mchezo wenye hadhi ya nyota tano umepigwa pale katika dimba la Anfield kati ya klabu ya Liverpool wenyeji wa mchezo dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City.

Mchezo huo mkali kabisa uliopigwa pale Anfield umeisha bila mbabe kupatikana kwani umemalizika kwa sare ya mabao baina ya wababe hao wa soka kutoka nchini Uingereza.liverpoolManchester City wakiwa ugenini waliuanza mchezo kwa kasi ya hali ya juu wakionekana wanataka kupata bao la mapema, Huku wakifanikiwa mpango kazi wao kwani John Stones aliwapa uongozi wageni hao mnamo dakika ya 23 ya mchezo.

Mchezo huo uliendelea kua wa kasi kwa pande zote kwani Liverpool nao walionekana kuamka na kuhitaji kupata goli ili kuweka mzani sawa, Lakini mambo hayakufanikiwa na mchezo kwenda mapumziko Man City wakiwa mbele kwa bao moja.

Kipindi cha pili mchezo uligeukia upande wa Liverpool ambapo walipeleka mashambulizi sana kwenye lango la City mpaka kupeleka kupata penati iliyowekwa kimiani na Alexis Macallister dakika ya 50 tu ya mchezo, Lakini hawakuishia hapo kwani waliendelea kuliandama lango la City.liverpoolBaada ya mchezo kati ya Man City na Liverpool kumalzika kwa matokeo ya sare leo imekua faida kwa klabu ya Arsenal ambao wameendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama zao 64 wakiwa sawa na Liverpool, Lakini Arsenal wakiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Man City wakiwa nafasi ya tatu na alama zao 63.

Acha ujumbe