Klabu ya Liverpool imeendelea kua na wakati mgumu ndani ya msimu huu baada ya kuishuhudia ikidondosha alama tatu dhidi ya klabu ya Brighton kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.
Klabu ya Liverpool imekubali kichapo cha mabao matatu kwa bila dhidi ya Brighton mchezo uliopigwa katika dimba la American Express Community. Klabu hiyo imekua na wakati mgumu msimu huu kutokana na matokeo ambayo wamekua wakiyapata.
Klabu ya Brighton wameweza kuifunga klabu ya Liverpool mabao matatu kwa bila huku wakiweza kucheza mpira mkubwa dhidi ya vijogoo hao wa Anfield, Mabao ya Brighton yote yalipatikana kipindi cha pili huku yakiwekwa kimiani na Solly March aliefunga mabao mawili pamoja na Danny Welbeck aliefunga bao moja.
Klabu ya Liverpool imekua kwenye wakati mgumu msimu huu lakini licha ya kua na msimu mbovu klabu hiyo inaandamwa na majeraha zaidi kwa wachezaji wake muhimu, Na hii inaweza kua sababu ya klabu hiyo kufanya vibaya zaidi msimu huu.
Vijogoo wa Anfield mpaka sasa wanashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama zao 28, Huku wakiwa wameachwa kwa pengo la alama saba na timu inayoshika nafasi ya nne klabu ya Newcastle United hivo mlima unaendele kua mgumu kuelekea mbio za kutafuta nafasi nne za juu.


