Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake.

Klabu ya Liverpool wamepunguza pengo la alama kati yao na Manchester City katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) hadi pointi tatu pekee baada ya kuwafunga Brighton 2-0 kwenye dimba la American Express.

Luis Diaz aliendelea kuwa mwiba eneo la ushambuliaji baada ya kulazimisha goli la kichwa dakika ya 19 ya mchezo na kuwapa Liverpool uongozi katika kipindi cha kwanza.

 

Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake.

Reds waliandika bao la pili kupitia mkwaju wa penati uliowekwa wavuni na mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah katika dakika ya 61 ya mchezo mnamo kipindi cha pili baada ya kiungo mkabaji Yves Bissouma kuunawa mpira ndani ya boksi.

Liverpool wanakuwa wameshinda mechi nane mfululizo EPL wakifukuzia ubingwa dhidi ya City wakati Salah akiandika goli la 20 na kufanya kuwa moja ya wachezaji watano katika historia ya EPL kufunga magoli 20+ katika miaka minne mfululizo.

Baada ya kipigo hicho, Brighton wanakuwa wamepoteza michezo mitano mfululizo katika ligi na kuteremka mpaka nafasi ya 13 wakiwa na alama 33 wakiwa sawa na Leicester city na Crystal Palace.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

CHEZA HAPA

Acha ujumbe