Liverpool Kuendelea Moto leo Au City Kufufuka

Kunako ligi kuu ya Uingereza leo utapigwa mchezo mkali kati ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Liverpool ambao watakua nyumbani katika dimba lao la Anfield kuwakaribisha klabu ya Manchester City.

Swali ni kwamba Liverpool wataendelea fomu yao bora waliyokua nayo msimu huu au klabu ya Manchester City wanaweza kufufukia kwa vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza, Kwani Man City hawajafanikiwa kushinda michezo yao sita ya mwisho kwenye michuano yote mitatu kwenye ligi ya Uingereza.liverpoolMabingwa mara 18 wa ligi kuu ya Uingereza majogoo wa Anfield ni wazi wao ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo kutokana na ubora ambao wamekua nao msimu huu, Lakini faida ya kua katika dimba lao la nyumbani mahali ambapo kumekua kama jahanamu kwa wapinzani wao wengi.

Vijana wa Pep Guardiola wanaweza kuamka leo na kupata matokeo dhidi ya Liverpool kwani wachezaji wao kadhaa waliokua majeruhi wamerejea kwenye kikosi, Hivo unaweza kua mchezo mgumu kwa vinara wa ligi kwani mchezo baina ya timu hizi mara nyingi unakua mchezo mgumu lakini wenye kuvutia kwelikweli.

Acha ujumbe