Klabu ya Liverpool inakusudia kufungua mazungumzo ya mkataba mpya na kipa wao, Alisson Becker atakaporudi klabuni baada ya msimu wa joto.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kwa sasa yupo akijiandaa na Copa America na ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao klabu inataka kuanza mazungumzo nao.

Alisson, 28, alijiunga na The Reds kutoka AS Roma kwa mkataba wa miaka sita mwaka 2018 kwa pauni milioni 66.8; Hiyo ilimfanya kuwa Kipa ghali zaidi ulimwenguni wakati huo, na ameshinda Ligi ya Mabingwa na Premier League.

Alisson alifunga bao la ushindi muhimu dakika za jioniii dhidi ya West Brom mnamo Mei na akashinda tuzo ya klabu kwa goli bora la msimu, akiwa kipa wa sita kufunga bao la PL na wa kwanza kufanya hivyo kwa kichwa – Alisson ameichezea Liverpool mechi 130.

Liverpool ilikuwa na msimu mgumu baada ya kushindwa kutetea taji lao la PL lakini walipata kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mbindee baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace kwenye siku ya mwisho ya msimu wa Premier League.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa