Klabu ya Liverpool ya Uingereza imesema kuwa haina mpango wa kumrejesha Arthur Melo katika Juventus mwezi Januari licha ya kuwa na tetesi huko Italy kuwa anarejea. Arthur anafanya kazi kwa bidii klabuni hapo ili apate kucheza.

 

Liverpool Kuhusu Arthur Melo

Ikumbukwe kuwa Liverpool walimchukua mchezaji huyo kutoka Juventus kwa mkopo ambapo angeenda kutumikia Majogoo hao kutokana na viungo wa timu hiyo kupata majeraha ya muda ambayo yamewafanya kukosekana kwa muda uwanjani.

Kutokana na majeraha hayo ndipo sasa Jurgen Klopp ambae ni kocha mkuu wa timu hiyo akaamua dirisha hilo kubwa lismpite bila kufanya maamuzi ya haraka ya kumpata kiungo atakayeisaidia timu hiyo huku kina Alcantara, Jota na Keita wakiendelea na matibabu ili warejee uwanjani.

 

Liverpool Kuhusu Arthur Melo

Arthur amekuja katika klabu hiyo huku wakiwa na matokeo ya kusua sua kwani hawatabiriki kama leo watashinda mechi ijayo ni sare na kuendeleza na mpaka Liverpool wamepoteza mchezo mmoja tuuh kwenye ligi ambao ni ule waliocheza dhidi ya Manchester United.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa