Liverpool Mbioni Kuwapiga Kikumbo Madrid

Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuwasiliana na nyota wa PSG, Kylian Mbappe juu ya upatikanaji wake wakati nyota huyu akitajwa kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Real Madrid.

Mkataba wa sasa wa nyota huyu wa Ufaransa unaisha mwezi Juni mwakani, na tayari Real Madrid walikuwa wanataka kuipata saini ya staa huyu katika dirisha hili la uhamisho mara baada ya michuano ya EURO 2020.

Kylian Mbappe PSG to Liverpool?

Liverpool pia wamekuwa wakihusishwa na staa huyu kwa kipindi cha miezi 12 sasa, na ripoti zinasema kuwa tayari wamewasilisha ombi la kufahamu ikiwa nyota huyu yuko wazi kuhamia klabu hiyo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa klabu ya Klopp inaweza kulazimika kuwauza baadhi ya wachezaji, kabla ya kuweza kukamilisha uhamisho wa Kylian Mbappe.

Hata hivyo, ripoti zinaonesha kuwa Kylian Mbappe mwenyewe anapendelea zaidi kuhamia Real Madrid, hivyo miamba hawa wa Hispania wanaonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuinasa saini yake ukilinganisha na Liverpool.


 

USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe