Liverpool Mipango yao kwa Zubimendi

Klabu ya Liverpool inaelezwa kuingia sokoni kutafuta kiungo wa ulinzi na katika machaguo yao ni kiungo wa klabu ya Real Sociedad Martin Zubimendi ambaye wanamuhitaji.

Liverpool mpaka sasa hawajafanya usajili wa mchezaji hata mmoja kwenye kikosi chao kuelekea msimu wa 2024/25 hivo kuacha maswali kwa wapenzi wa klabu hiyo, Lakini taarifa zinaeleza kua Martin Zubimendi unaweza kua usajili wa kwanza wa klabu hiyo kuelekea msimu mpya.liverpool

Martin Zubimendi ni moja ya viungo bora sana katika eneo la ulinzi na kuchezesha timu ambapo amekua akifukuziwa na vilabu kadhaa barani ulaya, Man United, Arsenal, pamoja na Barcelona ni vilabu ambavyo vinatajwa kunyemelea saini ya kiungo wa kimataifa wa Hispania kwa muda mrefu.

Klabu ya Liverpool licha ya kumuweka kiungo Martin Zubimendi kwenye orodha ya juu kabisa kwa wachezaji ambao wamelenga kuwapata katika majira haya ya joto, Lakini majogoo hao wa Anfield wanapaswa kutambua wana upinzani mzito kutoka kwa vilabu ambavyo nimevitaja hapo juu kwakua na wenyewe wanahitaji huduma ya mchezaji huyo.

Acha ujumbe