Klabu ya Liverpool ambae ipo chini ya kocha wake mkuu Jurgen Klopp leo itakuwa nyumbani Anfield kumkaribisha Ajax kwaajili ya kucheza mchezo wake wa pili wa Ligi ya Mabingwa baada ya kupoteza kwenye mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Napoli.

 

Liverpool Kujiuliza Dhidi ya Ajax

Liverpool leo hii itakuwa ni mechi yake ya kujiuliza kama ataweza kuendelea kwenye michuano hii ya UEFA kwani amekuwa akipitia wakati mgumu toka msimu huu uanze licha ya kushinda ushindi mkubwa wa ligi dhidi ya FC Bournemouth.

Klopp amekuwa hana furaha kwa matokeo anayoyapata kwenye klabu yake kutokana na wachezaji wake muhimu kupata majeraha mfano kina Konate, Alcantara, Jota na wengine wengi kiasi kwamba akalazimika kusajili kiungo kutoka Juventus kwa mkopo lakini hiyo ikawa haitoshi. Na taarifa imetoka jana Robertson hatakuwepo kwenye mchezo wa leo.

 

Liverpool Kujiuliza Dhidi ya Ajax

Ajax mechi yao ya kwanza ya ufunguzi wa klabu bingwa wameshinda ushindi wa kuridhisha wa mabao 4-0 dhidi ya Rangers na kuwa ni vinara kwenye kundi A, wakifuatiwa na Napoli ambao nao walijishindia mabao manne, wakati Majogoo hali ikiwa mbaya. Leo sasa watavaana na wababe wa Netherlands.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa