Liverpool wamewasilisha ofa ya awali ya £26m kwa nyota wa Roma Lorenzo Pellegrini, wakati wakitafuta mbadala wa Georginio Wijnaldum.

Pellegrini amemvutia Jurgen Klopp kwa kufanya kwake vizuri msimu uliopita, Liverpool wanaamini atakuwa mrithi mzuri wa Wijnaldum anayeondoka klabuni hapo.

Staa huyu aliwafungia Roma magoli 11 na kutoa usaidizi wa magoli mengine tisa kwa michuano yote msimu uliopita.

lorenzo pellegrini as roma

Akiwa na mwaka mmoja tu uliosalia kwenye mkataba wake, inaaminiwa kuwa Roma watalazimika kumuuza staa huyu wa miaka 24 kwenye dirisha la uhamisho la msimu huu wa joto.

Kwa mujibu wa Corriere dello Sport, Liverpool imekuwa klabu ya kwanza kuwasilisha ofa ya kumsajili staa huyu, na hili ni jaribio kwa Roma ambao wanaonekana bado wanamuhitaji.

Hata hivyo, klabu hii ya Serie A chini ya Meneja Jose Mourinho, inatarajiwa kuwa itaendelea kumshikilia staa huyu ili kupata ofa kubwa zaidi.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa