Liverpool wanaandaa mpango wa kuhakikisha mustakabali wa muda mrefu wa Rio Ngumoha, huku winga huyo kijana akitarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano mara atakapofikisha umri wa miaka 18 baadaye mwezi huu.

Kwa mujibu wa Paul Joyce wa The Times, Ngumoha pia atapewa ongezeko kubwa la mshahara, likiwa ni zao la maendeleo yake ya haraka ambayo yamemfanya kuwa mchezaji halisi wa kikosi cha kwanza.
Na kwa kuzingatia jinsi safari yake akiwa Liver ilivyokua kwa kasi, ni vigumu kusema kwamba hastahili kupewa mkataba huo mpya na maslahi hayo bora.
Ngumoha amepiga hatua kutoka kuwa kipaji cha kusisimua katika akademi hadi kuwa mchezaji ambaye mashabiki wa Liver kwa kweli wanatarajia kumuona mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
Mtindo wake wa uchezaji usio na woga tayari umemfanya kuwa kipenzi cha mashabiki. Anataka kuwakabili mabeki moja kwa moja.
Na pengine jambo muhimu zaidi ni kwamba haonekani kuogopa kucheza dhidi ya wapinzani wenye uzoefu wa kiwango cha juu.
Huo ndio mtazamo ambao unautaka kutoka kwa winga kijana. Mkataba mpya wa miaka mitano ungekuwa tamko kubwa la imani kutoka Liverpool. Ngumoha atatimiza miaka 18 Agosti 29, jambo litakalomwezesha kusaini mkataba mrefu zaidi wa kitaalamu.
Inaripotiwa kwamba mkataba huo mpya utaendelea hadi mwaka 2031. Hii ni Liverpool ikisema: “Hatumuoni tu kama kijana mwenye kipaji na anayetoa matumaini. Tunamuona kama sehemu ya mustakabali wetu.”




