Klabu ya Liverpool leo rasmi imefanikiwa kufuta uteja kwa klabu ya Brighton Hove and Albion baada ya kufanikiwa kupata matokeo ya ushindi wa mabao mawili kwa moja mapema leo.
Liverpool wakiwa katika dimba lao la Anfield walionekana kama wanaweza kuendeleza uteja wao mbele ya Brighton, Kwani mapema tu dakika ya 2 ya mchezo Danny Welbeck aliitanguliza Brighton mbele kwa bao moja.Vijana wa Jurgen Klopp walicharuka na kuanza kulisakama lango la Brighton mpaka pale walipofanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Luis Diaz dakika ya 27 ya mchezo na mchezo kufanikiwa kwenda mapumziko kwa sare ya goli moja kwa moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku vijana wa Klopp wakionekana wanaitaka mechi kwelikweli wakipeleka mashambulizi kwenye lango la Brighton mara kwa mara mpaka pale Mohamed Salah dakika ya 65b alipofunga goli la pili na la ushindi katika mchezo huo.Katika michezo minne ya mwisho waliyokutana Liverpool hawakua wamepata matokeo ya ushindi mbele ya Brighton, Lakini leo wamefanikiwa kufuta uteja na kushinda mchezo licha ya kushinda mchezo lakini inawapa fursa ya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama zao 67.