Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila mbele ya mahasimu wao klabu ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ulipigwa mapema leo katika dimba la Anfield.
Liverpool wamepata ushindi huo katika mchezo mgumu wa derby ya Merseyside dhidi ya Everton, Huku shujaa wa mchezo huo akiwa winga wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah aliefunga mabao yote mawili.Majogoo hao wa Anfield walianza mchezo kwa kasi sana wakionekana kutaka kupata bao la mapema zaidi, Lakini Everton walionekana kuzuia vizuri licha kucheza pungufu kwa muda mrefu wa mchezo baada ya beki wao Ashley Young kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya mchezo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika ubao ukisoma bila bila ambapo vijana wa Jurgen Klopp walikuja kipindi cha pili na msako wa hali ya juu wakifanya mashambulizi mara kwa mara langoni kwa Everton, Mpaka dakika ya 75 walipopata mkwaju wa penati na kuwekwa kimiani na Mohamed Salah.Klabu ya Liverpool licha ya kupata bao moja lakini hawakuridhika mpaka pale dakika ya 98 ya mchezo ambapo walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Mohamed Salah baada ya kufanya shambulizi la kushtukiza, Klabu hiyo ilifanikiwa kushinda kwa mabao hayo mawili na kupanda kileleni mwa msimamo wakiwa na alama zao 20.