Liverpool Yamfukuzia Bremer kama Mbadala wa Van Dijk

Klabu ya Liverpool ipo kwenye mchakato wa kutafuta mbadala wa beki wao wa kimataifa wa Uholanzi Virgil Van Dijk ambapo macho yao yamegota kwa beki wa kimataifa wa Brazil Gleison Bremer anayekipiga Juventus.

Bremer amekua na muendelezo mzuri wa kiwango bora jambo ambalo lilifanya klabu ya soka ya Juventus kumsajili kutoka klabu ya Torino ya huko huko nchini Italia, Beki huyo amekua ndani ya Juventus kwa misimu miwili sasa na kiwango chake kimeendelea kua kizuri na kuanza kupata nafasi kwenye timu ya taifa ya Brazil.liverpoolKlabu ya Liverpool inamuona beki Van Dijk kama yuko mwishoni kwenye ubora wake hivo wameanza kutafuuta mbadala wa beki huyo mapema, Jina ambalo limeongoza orodha ya wachezaji wanaotakiwa kuvaa viatu vya Van Dijk ni beki huyo raia wa kimataifa wa Brazil.

Kumpata Gleison Bremer kutoka ndani ya klabu ya Juventus haitakua rahisi kwa klabu ya Liverpool kwani Juventus pia hawatakua tayari kumpoteza beki huyo, Lakini hii ni azma ya majogoo wa Anfield kuhakikisha wanapata huduma ya beki huyo wa kimataifa wa Brazil kinachosubiriwa ni kuona ofa ambayo wataituma kwa klabu ya Juventus.

Acha ujumbe