Klabu ya Liverpool imethibitisha kukamilisha uhamisho wa beki wao Sepp van den Berg kwa mkopo wa muda mrefu kwenda klabu ya FC Schalke 04 inayoshiriki Ligi ya Bundersliga ya nchini Ujerumani.

Liverpool Yamtoa kwa Mkopo Sepp van den Berg

Taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hizo mbili zinaonesha kuwa tayari kuna makubaliano kati yao, huku Liverpool wakimtakia kila la heri mchezaji wao ambaye ataenda kuanza maisha mapya akiwa na miamba hiyo ya Ujerumani.

Liverpool Yamtoa kwa Mkopo Sepp van den Berg

Van den Berg, ambaye amecheza mechi nne za wakubwa akiwa na majogoo tangu uhamisho wake wa paundi Milioni 4.4 kutoka PEC Zwolle mwaka 2019, alitumia msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Preston ambako alicheza michezo 50 katika mashindano yote.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa