Liverpool Yatupwa nje FA

Klabu ya Liverpool imetupwanje kwenye michuano ya kombe la FA ya nchini Uingereza baada ya kukubali kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya klabu ya Brighton and Hove Albion.

Klabu ya Brighton imeitupa nje klabu ya Liverpool kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha mbao mawili kwa moja, Huku Kaoru Mitoma akizamisha ndoto za vijogoo dakika za lala salama na kuwafanya Brighton kusonga mbele kwenye michuano hiyo.LiverpoolMabingwa hao watetezi wa kombe hilo kwasasa wamebakia kwenye mataji mawili msimu huu ambayo ni ligi kuu ya Uingereza na ligi ya mabingwa ulaya, Huku wakiwa hawana uhakika wa kubeba taji hata moja kati ya hayo na wakiondoshwa kwenye makombe mawili ambayo walikua ndio mabingw watetezi.

Klabu ya Liverpool imekua kwenye wakati mgumu zaidi msimu huu kwani msimu uliomalizika walikua wanagombania makombe yote manne mpaka dakika za mwisho, Lakini msimu huu mpaka sasa wamebaki kwenye makombe mawili ambayo pia hawapewi nafasi ya kuyachukua kutokana mwenendo wao.LiverpoolLiverpool inakamata nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa wanakwenda kukutana na Real Madrid kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya 16 bora, Hii ni wazi kua klabu hiyo ipo kwenye kipindi kigumu msimu huu kuliko msimu wowote ndani ya miaka mitano ya hivi karibuni.

Acha ujumbe