Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Luis Nani, 35, amejiunga na kikosi cha Venezia kinachoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mpaka mwaka 2023.
Nyota huyo aliyechezea Man United mara 230 kati ya 2007 na 2015 amesajiliwa rasmi ya Venezia kwa mkataba wa miezi 18. Alifunga mabao 41 na kuchangia mengine 73 katika kipindi hicho cha miaka minane akiwa Old Traford.
Venezia wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa jedwali la Serie A na wanapambana kutoka kwenye hatari ya kushushwa daraja mwishoni msimu huu wa 2021-22.
Luis Nani alishinda taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na Europa League. Amewahi pia kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na matatu ya Ligi Kuu ya Ureno akichezea Sporting Lisbon.
Luis amechezea vilabu vya Manchester United, Fenerbahce, Valencia, Lazio na Orlando katika Major League Soccer (MLS) mpaka sasa anajiunga na Venezia.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA