Habari njema kwa mashabiki wa Atletico Madrid na La Liga kwa ujumla, Luis Suarez kurejea tena uwanjani baada ya kupona COVID19.

Suarez alikosekana kwenye michezo 4 ya Atletico baada ya kupata maambukizi ya COVID19 alipokuwa na timu ya taifa mwezi uliopita.

Taarifa rasmi kutoka Atletico Madrid zimethibitisha – Luis Suarez atajiunga na wachezaji wenzake kwenye uwanja wa mazoezi kuanzia leo (Ijumaa) baada ya vipimo kuonesha amepona ugonjwa huo (COVID19).

Luis Suarez, Luis Suarez Kurejea Uwanjani Wiki Hii., Meridianbet
Suarez Akiwa Mazoezini Atletico Madrid

Luis Suarez atajiunga na mazoezi ya kikosi cha kwanza kesho (Ijumaa) baada ya kukutwa hana maambukizi ya COVID19 kwenye vipimo maalumu vya La Liga PCR.

“Baada ya kupona COVID19 na kufuata taratibu zote za afya, atajumuishwa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza na atakuwa chini ya uangalizi wa kocha – Diego Simeone.” Taarifa rasmi kutoka Atletico Madrid iliripoti siku ya Alhamisi.

Simeone atafanya maamuzi kama atamtumia Suarez kwenye mchezo dhidi ya Real Valladolid siku ya Jumamosi au ataamua kumpumzisha, maamuzi haya yatategemea hali ya utayari kwa mshambuliaji huyu raia wa Uruguay.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Luis Suarez, Luis Suarez Kurejea Uwanjani Wiki Hii., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

24 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa